
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola amefiwa na mkewe Mary.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu
wa Rais imesema Mary amefariki dunia leo Jumatatu Januari Mosi, 2018
jijini Dar es Salaam.
Wakati huohuo, Ofisi ya Bunge katika
taarifa kwa umma imesema Spika Job Ndugai amemtumia rambirambi Lugola
kutokana na kifo cha mkewe.
Imeelezwa msiba upo Railway Club Gerezani jijini Dar es Salaam.
Ndugai ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza mpendwa wao.

Post a Comment
karibu kwa maoni