0
Responsive imageWatu kumi na tisa wameripotiwa kufa tangu kuanza kwa msimu wa baridi kali na kuanguka kwa theluji katika maeneo mbalimbali ya mashariki mwa Marekani.
Taarifa kutoka nchini humo zinaarifu kuwa bado kumekuwa na hali ya baridi kali na theluji katika maeneo ya makazi na yale ya huduma za kijamii ambapo baadhi ya watu wameondolewa katika makaazi yao ili kuepuka maafa zaidi yanayoweza kujitokeza.
Idara ya Taifa ya Utabiri wa hali ya Hewa nchini Marekani (NWS) imetahadharisha kwamba hali ya  baridi na kuanguka kwa theluji  itaendelea kuwa mbaya mashariki mwa Marekani.
Usafiri wa umma na safari za mashirika mbalimbali ya ndege umeathiriwa kutokana na hali hiyo huku juhudi mbalimbali za kuuondoa theluji katika miundombinu ya barabara na viwanja vyandege zikiendelea kufanyika.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top