Akizungumza na WALTER HABARI mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa
Manyara Lawrence Tara amesema hali hiyo inawafanya viongozi wa Chama hicho
kufanya kazi kwa woga akieleza kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka.
Wameyazungumza hayo wakiwa katika kikao chao cha baraza la
viongozi mjini Babati.
Tara alisema January 12.2018 Mkuu wa wilaya ya Hanang Sarah
Msafiri amewaweka ndani madiwani watatu kwa madai ya kushindwa
kuhamasisha maendeleo kwenye kata zao,amewataja madiwani waliokamatwa ni Peter
Loy diwani wa Katesh mjini,Hashim Khamunga diwani wa Endasaki,Diwani wa kata ya
Dirma Faustin Kamsinda na hivi karibuni amemtia ndani mwenyekiti na
diwani wa Basodesh Mchungaji Michael Boay.
Naye mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa CHADEMA [BAWACHA]
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Babati mjini mheshimiwa Paulina Philipo
Gekul amesema kuwa Mkuu wa mkoa ni mdogo kwa umri na hajui wajibu wake
kwani anachokifanya inaonyesha wazi kuwa hajasoma katiba ya nchi inasema nini.
Amesema mkuu wa mkoa anafanya kazi za mkurugenzi na kazi ya
katibu mwenezi wa Ccm mkoa.
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti. |
"Kwa hiyo mkuu wetu wa mkoa hafiti kabisa na hajui
anachokifanya na mpaka sasa hajawahi kufanya kazi ya ukuu wa mkoa,sasa kama
Rais atamuacha atapata majibu mapema sana, aliongeza Gekul.
Akiwa katika mkutano wa hadhara kata ya Haydom wilayani
Mbulu juzi Januari 11.2018 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander
Mnyeti aliwataka madiwani wa vyama vya upinzani kujiunga na CCM ili waweze
kushirikiana naye kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama tawala.
Alisema yupo tayari kupokea simu ya diwani wa CCM hata
akipigiwa usiku wa manane, ili kumpa msaada lakini si diwani kutoka vyama
vya upinzani.
Alisema diwani wa Chadema ni ngumu kufanikisha maendeleo
ya wananchi kwa madai kuwa, hakuna ambaye atamsikiliza akiwasilisha hoja zake
katika vikao vya halmashauri husika.
"Hata hapa Haydom najua ni ngome ya
Chadema hata mwenyekiti wa kijiji namuona ana damu ya CCM, sasa ondokeni huko
mje huku tutekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 kwa kuleta
maendeleo," alisema Mnyeti.
Pia, aliwataka watumishi wa halmashauri hiyo kutekeleza
na kufanikisha kwa vitendo ilani ya CCM hata kama hawana kadi ya chama hicho
kwani ndicho ambacho kipo madarakani.
Ikumbukwe kuwa Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kuagiza
kukamatwa kwa mtu na kuwekwa rumande yako chini ya vifungu vya 7 (mamlaka ya
mkuu wa mkoa) na 15 (mamlaka ya mkuu wa wilaya) vya Sheria ya Tawala za Mikoa,
1997. Vifungu hivyo vinafanana katika uandishi na hata mantiki isipokuwa tu
maneno 'Mkuu wa Mkoa' na 'Mkuu wa Wilaya'.
Pia, kama Mkuu wa Mkoa au Wilaya ana sababu za kuamini kuwa
mtu yeyote aweza kuvunja amani au kuharibu utulivu uliopo au kufanya kitendo
chochote ambacho kinaweza kuvunja amani au kuharibu utulivu na uvunjifu huo
hauwezi kuzuiwa kwa njia yoyote nyingine isipokuwa kumsweka rumande mtu huyo,
Mkuu wa Mkoa au Wilaya aweza kuagiza kwa maneno au maandishi kukamatwa kwa mtu
huyo.
Mtu aliyekamatwa kwa amri au maelekezo ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya jinai. Endapo hatafikishwa Mahakamani kwa muda unaopaswa, na muda kuisha, anapaswa kuachiwa na hapaswi kukamatwa tena kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya kwa namna ile ile.
Wakati wa kuagiza kukamatwa kwa mtu yeyote au muda mfupi baada ya kuagiza, Mkuu wa Mkoa au Wilaya lazima aandike sababu za kukamata au kuagiza kukamatwa kwa mtu husika na kupeleka nakala kwa Hakimu ambaye mbele yake aliyekamatwa atafikishwa kwa ajili ya kushtakiwa.
Mtu aliyekamatwa kwa amri au maelekezo ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya jinai. Endapo hatafikishwa Mahakamani kwa muda unaopaswa, na muda kuisha, anapaswa kuachiwa na hapaswi kukamatwa tena kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya kwa namna ile ile.
Wakati wa kuagiza kukamatwa kwa mtu yeyote au muda mfupi baada ya kuagiza, Mkuu wa Mkoa au Wilaya lazima aandike sababu za kukamata au kuagiza kukamatwa kwa mtu husika na kupeleka nakala kwa Hakimu ambaye mbele yake aliyekamatwa atafikishwa kwa ajili ya kushtakiwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni