
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa
amewapongeza maaskofu kwa kuunga mkono mambo aliyosema wamekuwa
wakiyapigania.
Lowassa
ametoa pongezi hizo jana Februari 11,2018 akimnadi mgombea ubunge
jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu katika Kata ya Kijitonyama.
“Leo
kwenye magazeti wameandika kwamba Baraza la Maaskofu wamezungumzia
mambo ambayo tumekuwa tunayasema kila siku, kuhusu kuzuia uhuru wa
kuzungumza na suala la maadili. Ninawashukuru sana maaskofu,
ninawapongeza sana kwa kuunga mkono ambayo tumekuwa tunayasema,” alisema
Lowassa.
Baraza
la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limetoa ujumbe wa Kwaresima wa
mwaka 2018 ndani yake likitoa msimamo kuhusu masuala ya kisiasa,
kiuchumi na kijamii nchini.
Lowassa
akimnadi Mwalimu alisema anamfahamu kwamba ni kijana shupavu na mchapa
kazi ambaye akipewa kura wananchi wa Kinondoni watapata maendeleo.
“Kinondoni msilale mpaka kieleweke. Mchagueni Salum Mwalimu akawaletee maendeleo,” alisema.
Mwalimu akiomba kura alisema Kinondoni ni watu ambao wanajitambua.
“Kinondoni
ni watu mnaojitambua, ni watu ambao mlijitoa mwaka 2015, wengine
waliachika. Ninawapenda sana, ninajua nina deni kubwa la kuwalipa,”
alisema.
Mwalimu
alisema, “Ninapozungumza najua ninazungumza na wajanja ambao
hawadanganyiki. Tangu juzi, wenzangu wameleta fedha hapa Kijitonyama kwa
ajili ya kununua shahada.”
Alisema waliposikia anagombea ubunge walipata hofu kubwa, vikao vikawa haviishi wakitafakari itakuwaje nikienda bungeni.
Post a Comment
karibu kwa maoni