0
Na Kennedy Lucas,Kilimanjaro.
Image result for UZUNGUNI FC HAI 
Timu ya Uzunguni fc kutoka Hai inatarajia kumenyana vikali Leo  na timu ya Forest fc kutoka Siha katika mchezo wa fainali ya ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro utakaopigwa kwenye dimba la Mawalimu Nyerere Complex Bomang'ombe wilaya ya Hai.
Mchezo huo unatarajia kuwa mkali na wakuvutia kutokana na ubora wa vikosi vyote ukiangalia kuanzia walipoanza hatua ya makundi ya michuano hiyo mpaka wakaingia nane bora moto ulikuwa ni ule ule uliowashwa mwanzo.
Akiongea na championi mwenyekiti wa timu ya Forest fc Hassan Kipingu alisema mpaka sasa vijana wake wako katika hali na morali nzuri kuhakisha wanashinda mchezo wa kesho kwani wako vizuri kuliko wapinzani wao.
"Niwaambie tu mashabiki wetu kuwa wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao na sisi tunawahidi hatutowaangusha tutapambana mpaka tuwe mabingwa"alisema Kipingu.
Kwa upande wake katibu wa Uzunguni fc Abdul Iddy alisema wamefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo hivyo hana wasiwasi wa aina yoyote na vijana wake huku akiweka wazi kuwa licha ya wapinzani wao kuwa wazuri lakini kwao watakaa tu.
" Mashabiki wategemee ushindi kwa sababu tangu mwanzo timu ilianza kwa moto na hatujauzima bado utaendelea kuwaka mpaka ligi ya mabingwa mikoa (RCL)"alisema Iddy.
Uzunguni fc wametinga fainali baada ya kuichapa Upendo fc ya Siha goli 1-0,wakati Forest fc imetinga hatua hiyo baada ya kuifumua Golden heroes ya Moshi manispaa mabao 3-0

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top