Bonanza la michezo la waalimu wa shule za Msingi na sekondary mji wa Babati inatarajiwa kufanyika leo huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa mkuu wa wilaya Babati Raymond Mushi.
Ofisa utamaduni wa mji wa Babati Isaack Sawala alisema maandalizi ya bonanza hilo lililopewa jina la Teachers Sports day litakalofanyika katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati kwa kushirikisha waalimu wote wa shule za msingi na sekondari yamekamilika kwa kiasi kikubwa na lengo lake likiwa ni Kukutanisha waalimu,kufahamiana na kuendelea kuisapoti michezo ndani ya mkoa wa Manyara.
Alisema itakuwepo michezo mbali mbali kama mpira wa pete,mpira wa wavu,riadha mita 100,kukimbia na kamba,kukimbia na gunia pamoja na mchezo wa bao na kuweka wazi kuwa zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi wa kwanza hadi wanne.
"Niombe tu waadau waendelee kutuunga mkono katika juhudi zetu hizi za kuisapoti michezo ndani ya mkoa wa Manyara na wao waige tunachokifanya hili waweze kuinua na kuendeleza vipaji" alisema Sawala.
Alizitaja timu zitakazoshiriki kwenye mchezo wa mpira wa miguu katika bonanza hilo kuwa ni Waalimu wa Sekondari,waalimu wa msingi,Hospitali ya Mrara na timu ya Halmashauri ya mji wa Babati.
Kwa upande wa wadhamini alisema bonanza hilo limedhaminiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),benki ya NMB,benki ya CRDB,benki ya Afrika (BOA),Vodacom,Alica studio, Sigema stationery, benki ya Posta,na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca cola.
Post a Comment
karibu kwa maoni