Mnamo
mwezi Julai 2017, Kampuni ya Progress rail Locomotives (PRL) ya
Marekani ilileta vichwa vya treni 11 katika Bandari ya Dar es salaa kwa
ajili ya kuviuza vyenye namba 9014, 9015, 9016, 9017, 9018, 9019, 9020,
9021, 9022, 9023 na 9024.
Tarehe
27 septemba, 2017 Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa aliteua kamati ya wataalamu kwa ajili kubaini
kama vichwa hivyo ni vipya au la.Wajumbe wa kamati hiyo walitoka chuo
kikuu cha Dar es salaam, TEMESA na shirika la Reli Tanzania (TRC).
Kamati
hiyo ilifanya kazi hadi 15 oktoba, 2017 na kukabidhi ripoti kwa
Mheshimiwa Waziri.Kamati ilibaini kuwa vichwa hivyo vya treni ni vipya.
Aidha
tarehe 16 Oktoba, 2017 Mheshimiwa Waziri kwa mara nyingine aliteua
kamati ya wataalamu wenye taaluma mbalimbali wakiwemo wanasheria
wahandisi na wachumi kwa ajili ya kujadiliana bei ya kuvinunua vichwa
hivyo.
Awali
mwaka 2015,Serikali ilinunua vichwa kama hivyo 13 vyenye namba 9001,
9002, 9003 ,9004,9005,9006,9007,9008, 9009 ,9010, 9011, 9012 na 9013
kwa bei ya dola za kimarekani Milioni 3,200,000 kwa kichwa kimoja.
Kamati
hivyo ilifanya majadiliano ya bei na kufikia muafaka wa kununua kwa
dola za kimarekani milioni 2,400,000 kwa kichwa kimoja ambavyo ni
pungufu ya dola 800,000 kwa kila kichwa cha treni kulinganisha na bei ya
vichwa tulivyonunua awali,kwa maana hiyo kwa vichwa 11 serikali imeokoa
dola 8,800,000.
Majaribio
yatakuwa katika awamu tatu.Kwanza ni ukaguzi kwa kuvitizama(visual
inspection),pili ni kuviwasha na kuvipa mizigo vikiwa havitembei(load
box) na tatu ni kufunga na kuvuta mzigo tani 700 toka Dar es salaam hadi
Morogoro na tani 1200 toka Morogoro hadi Kigoma na Mwanza.
Ununuzi
wa vichwa hivi 11 utaongeza ufanisi wa shirika kwani kwa sasa hivi
tunavyo vichwa 29 madhubuti kati ya vichwa 47 tunavyovihitaji ili kutoa
huduma nzuri kwa wateja wetu.
Post a Comment
karibu kwa maoni