SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua
mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na
vituo vya afya nchini.
Hayo
yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa
Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini jana
jijini Dar es salaam.
“Serikali
imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga
shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya
uchunguzi kwa haraka vya ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert ” alisema Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy alisema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya
Kifua Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure.
Aidha,
Waziri Ummy alisema kuwa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji
kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende
hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka.
Waziri Ummy alisema kuwa takribani watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016.
Sambamba
na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za
Genexpert kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna
maambukizi au hapana kwa hospitali za ,Kairuki, Agakhan, Regency , TMJ
na Indumandal ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .
Aidha
Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali
mara wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa
muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua
uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa mara.
Post a Comment
karibu kwa maoni