0
Image result for ccm tanzaniaChama cha Mapinduzi kimepata pigo baada ya kuondokewa na  Katibu wa Chama hicho wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Mwili wa Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Babati vijijni Edna Edmund aliefariki ghafla jana akiwa ofisini kwake  unaagwa leo kuelekea Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma  kwa ajili ya Mazishi.

Katibu wa Ccm mkoa wa Manyara  Paza Mwamlima amesema wamepokea kwa mshtuko kifo cha katibu huyo aliekuwa akiendelea na majukumu yake ya Chama na kwamba hakuwahi kuugua.

Viongozi mbalimbali kutoka Manyara na nje ya mkoa wanatarajiwa kuwepo katika kutoa rambi rambi zao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top