Watu
wasiojulikana wameovamia Maeneo ya katani na kufanya kilimo mpaka kuwafikia
mazao kufikia hatua ya kukomaa bila kujulikana na mamlaka husika.
Madiwani
wa Halmashauri ya mji wa Babati wamekutana Leo april 24.2018 katika kikao chao
kuwasilisha taarifa mbalimbali za maendeleo katika kata zao ambapo mjadala
mkubwa ilikuwa ni Uvamizi wa maeneo ya Maisaka katani.
Diwani
wa kata ya Maisaka Abrahamani Kololi amesimama na kuomba busara itumike kwa
kuwa kilichopo shambani ni chakula na sio bangi.
Hata
hivyo mwanasheria wa Halmashauri ya mji wa Babati akitolea ufafunuzi wa
kisheria kuhusu jambo hilo alieleza kuwa limeshakuwa la kisheria hivyo wasubiri
maamuzi yatakayotolewa kwamba yateketezwe au nini kifanyike.
Mpaka
sasa mazao yaliyopandwa katika maeneo hayo yanakaribia kukomaa hali inayowapa
wengi maswali iliwezekanaje watu kufanya kilimo,kupanda hadi kufanya palizi
bila kuonekana.
Post a Comment
karibu kwa maoni