Jumla
ya maofisa wa Jeshi la Polisi wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na
utovu wa nidhamu kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu.
Kauli
hiyo imetolewa jana Aprili 7 na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro
alipokuwa akizungumza mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa
nyumba 31 za Polisi na ufunguzi wa kituo cha Polisi cha Utalii na
Kidiplomasia jijini Arusha.
Sirro
alisema kazi ya Jeshi la Polisi ni kurekebisha mienendo ya wananchi,
hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri
wao kwanza.
Alifafanua
kwa kulitambua hilo ndiyo maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo
walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka
2015, 198 walifukuzwa kazi.
Alisema kwa mwaka 2016 walifukuzwa askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa askari 14.
“Hatuna muhali kuwachukulia hatua askari wanaokiuka utaratibu na nidhamu ya utendaji katika Jeshi la Polisi,” alisema IGP Sirro.
Post a Comment
karibu kwa maoni