Uongozi
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umesema kuwa unajipanga
kuhakikisha unaisaidia na Yanga katika mchezo wake wa marudiano wa Kombe
la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolayta Dicha utakaofanyika Aprili 18,
mwaka huu huko Ethiopia.
Lengo kubwa la TFF kufanya hivyo ni
kutaka kuiona Yanga inatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwani
ndiyo timu pekee iliyobakia msimu huu ambayo inaipeperusha bendera ya
Tanzania kimataifa.
Katika mechi ya juzi Jumamosi
iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar er es Salaam, Yanga
iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyoiweka katika nafasi nzuri ya
kutinga hatua hiyo ya makundi.
Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao,
alisema kuwa ili kuhakikisha timu hiyo inasonga mbele katika michuano
hiyo, wamejipanga vilivyo kuisaidia iweze kutimiza ndoto hiyo katika
mechi ya marudiano.
“Tutaipatia muda wa kutosha wa
maandalizi lakini pia tutatuma wawakilishi wetu Ethiopia kabla ya mechi
hiyo kwa ajili ya kwenda kuweka mambo sawa ili siku itakapoenda huko
isikumbane na usumbufu.
“Michuano hii ni ya kimataifa na
ikifanya vizuri sifa itakuwa siyo kwa klabu pekee bali kwa taifa zima la
Tanzania, kwa hiyo inatubidi tushirikiane nao kwa karibu kabisa ili
kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika mchezo wake huo wa marudiano,”
alisema Kidao.
Post a Comment
karibu kwa maoni