Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi Visiwani Zanzibar, Hassan Nassir Ali,
amefunguka juu ya uhamisho wake aliopewa siku chache baada ya kuwaonya
wanaume juu ya tabia zao zisizofaa kwenye jamii.
Kamanda
Hassan amesema kwamba uhamisho wake ni wa kawaida na wala haujatokana
na kauli alizotoa, ambazo zilizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.
Akiendelea
kutolea ufafanuzi suala hilo Kamanda Hassan amesema kwamba kauli hiyo
aliitoa na alikuwa anamaanisha, lakini haijaleta mtafaruku wowote kwenye
jamii kama ambavyo inasemekana, na hata walipoijadili kwenye Baraza la
Wawakilishi Zanzibar ilikuwa ni utani.
“IGP
amesema mwenyewe amefanya uhamisho na uteuzi huu ili kuimarisha safu
yake kiutendaji, mimi ningekuwa nimesema nimewakwaza watu sio kweli,
hata wale waliosema katika Baraza la Uwakilishi ilikuwa ni kwa utani, ni
uhamisho wa kawaida kabisa, wala sio chuki”, amesema Kamanda Hassan.
Kamanda
Hassan ameendelea kwa kuwataka wananchi wa Kaskazini Pemba ambako
amehamishiwa kufuata sheria bila shuruti kwani kazi iko pale pale.
“Nitaendelea
kufanya kazi yangu vizuri nitaendelea kusimamia sheria vizuri, kazi iko
pale pale bado mimi ni Kamanda wa polisi nitasimamia sheria za nchi,
wala sio jambo langu hili wala mie sio mzee wa vikohozi, mimi nimetoa
mifano, hivyo kazi iko pale pale”, amesema Kamanda Hassan.
Kamanda
huyo ambaye metokea visiwani Zanzibar wiki iliyopita aliibua mzozo
kwenye mitandao baada ya kuwaonya wanaume wenye tabia ya kukohoa pindi
waonapo wanawake wenye maumbile makubwa, akisema hilo ni kosa kisheria
ambalo linatambulika kama shambulio la aibu.
Post a Comment
karibu kwa maoni