Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule amethibitisha kufariki kwa
wagonjwa saba wa kipindupindu katika Wilaya ya Sumbawanga huku wagonjwa
wengine 44 wakibaki wodini kuendelea kupatiwa matibabu na wagonjwa 115
wakiruhusiwa kurudi nyumbani.
Akizingumzia
tukio hilo Dkt. Haule amesema kuwa ugonjwa huo umelipuka Mei 6, 2018
katika Kijiji cha Mayenje, kata ya Milepa katika bonde la Ziwa Rukwa na
kusambaa katika maeneo mengine ya Wilaya na hatimaye kupatikana kwa
wagonjwa wawili katika hospitali ya rufaa ya mkoa.
"Sasa
hivi katika bonde la ziwa Rukwa kuna shughuli za uvunaji wa mpunga na
hivyo watu wengi hutokea huku juu kwenda bondeni kutafuta vibarua vya
kuvuna mpunga kwenye maeneo hayo yaliyoathirika na kipindupindu, maji
yanayotumika huko ni machafu kutoka katika madimbwi na mito. Nawaomba
viongozi wa dini watoe tahadhari kwa waumini hasa katika maeneo yale
yalioathirika zaidi", amesema Dkt. Haule.
Post a Comment
karibu kwa maoni