Magavana wa nchi za
Afrika wametakiwa kuwa na utayari wa kuzisaidia nchi zao kutatua changamoto za kiuchumi
na kuhamasisha maendeleo endelevu ili kuendana na mapinduzi makubwa yanayotokea
kote Duniani kwa kuhamasisha ukuaji wa viwanda.
Rai hiyo imetolewa
na Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Dkt. Akinumwi
Adesina, wakati wa Mkutano wa 6 wa jukwaa la ushirikiano kati ya Jamhuri ya
Korea Kusini na Nchi za Afrika uliolenga kujadili namna bora ya kuchochea
ukuaji wa sekta ya viwanda katika Nchi za Afrika.
Wadau wa Mkutano
huo uliofunguliwa na Makamu wa Waziri Mkuu wa Korea Kusini Bw. Kim Dog – Yeon, wamezitaka nchi za Afrika
kuhakikisha zinafanya mapinduzi ya kiuchumi kwa kuwekeza kwenye viwanda na miundombinu kwa
kuwa itasaidia uchumi wa nchi kukua kwa
kasi na kuleta maendeleo yenye tija.
Vilevile nchi za
Afrika zinahitaji kuwa na na ushirikiano wenye manufaa na wahisani ikiwemo nchi
ya Jamuhuri ya Korea Kusini ili kuharakisha maendeleo hayo ya kiuchumi kwa
kubadilishana uzoefu na kubaini fursa za ukuaji wa uchumi utakaochochea
ushirikiano huo.
Afrika inafursa
nyingi za kukuza uchumi kwa kuwa inarasilimali za kutosha kwa takribani sekta
zote muhimu za maendeleo ikiwemo ya madini, kilimo, mifugo na Uvuvi.
Imetolewa
na;
Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini
Wizara
ya Fedha na Mipango
Post a Comment
karibu kwa maoni