0
Mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Babati Gerald Mtui alihudhuria katika ufunguzi wa ligi hiyo.
YOUNG BOYS imeanza vyema mashindano ya Ligi ya Mbuzi kwa kuwachapa waandaji VETA FC 2-0 kundia A katika uwanja wao wa Nyumbani.
Lengo la mashindano haya ni kudumisha Ujirani Mwema kati ya Chuo cha ufundi stadi Veta na wadau jamii inayoizunguka.
Mchezo huo uliochezeshwa na Waamuzi Martin Faustin akiwa kati kati na filimbi akisaidiwa pembeni na washika bendera Mohamedi Juma na Kaji Bessi mabao ya Young Boys yalipatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili.
Kocha  wa timu ya Young Boys  Shafii Abdala alisema kuwa Ligi ya Mbuzi ni ngumu kwani inashirikisha timu ambazo nazo zinahitaji kupata ushindi.
Kepteni wa timu ya Veta Fc Kais Junior mara baada ya mchezo kumalizika alizungumzia mchezo huo ambapo alisema waliweza kuwamudu wapinzani katika mchezo lakini hakuridhishwa na mwamuzi wa kati kwa madai kuwa alitoa penati ya upendeleo kwa upinzani iliyowapa bao pili.
Kipindi cha pili timu ya Veta Fc  ilianza kwa kasi kubwa ambapo ilifanya mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la Young Boys ila bahati haikuwa yao kwenye mchezo wa leo.
Mechi nyingine itapigwa kesho may 24.2018 ambapo  River Corner Fc akivaana na City Center na Mei 25 itakuwa zamu ya Friend Rangers Vs Young Boys.
Kauli mbiu ya ligi hii ni, USTAWI WA MAENDELEO YA VIJANA,KASI YA UFUNDI STADI.
Kumbuka kuwa mashindano hayo yakitumika vyema yatasaidia kuibua vipaji mbalimbali vijijini na kutengeza ajira kwa vijana.




Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top