0
Na Pamela Mollel, Arusha

Baadhi ya mahabusu wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi jijini Arusha leo wamegoma kushuka katika gari la magereza kwa madai kuwa hawatendewi haki kwa kesi zao kutosikilizwa hali inayowalazimu kukaa mahabusu kwa muda mrefu bila kujua hatima yao.

Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya mahakama majira ya saa 3:27 asubuhi ambapo tukio hilo lilisimamisha shughuli za mahakama kwa muda wa zaidi ya masaa mawili huku baadhi ya watuhumiwa wengine wa ugaidi wakivua nguo zao kushinikiza kesi zao kusomwa

Mahabusu 32 tu ndio waliokubali kushuka katika gari hilo na kuingia mahakamani huku 29 wakigoma kushuka na kubakia ndani ya gari hali iliyozua taharuki kwa baadhi wa watu walikuja kufatilia kesi hiyo na zinginezo.

Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Mhe. Nestory Baro aliwataka watuhumiwa hao kuwa wavumilivu, kwa kuwa kesi yao ipo katika hatua za mwisho huku akiwasii kutogomea kuja mahakamini kwa kufanya hivyo wanajinyima haki yao ya kisheria.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mahakamani hapo baadhi ya watuhumiwa Shabani Idi na Yusuph Alli waliiomba mahakama kuharakisha kesi hiyo kwa kuwa familia zao zinaishi katika wakati mgumu.

“Mtoto wangu wa darasa la nne amekatisha masomo anaokota makopo kwa ajili ya kuuza ili familia wapate chakula pamoja na wadogo zake kupata nauli ya shule”alisema Shabani.


Waliongeza kuwa familia zao sasa zipo hatarini kuingia katika makundi mabaya ya tabia kutokana na wazazi wao kuwa mbali nao hivyo wao kuendelea kuwepo magerezani ni changamoto kubwa sana kwa familia zao

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top