RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, ametangaza
msamaha kwa Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza
(Papii Kocha) ambao waliofungwa maisha katika Gereza la Ukonga jijini
Dar es Salaam na kutaka waachiwe huru mara moja kutoka gerezani.
“Tanzania
tuna jumla ya wafungwa 39,000 ambapo wanaume ni 37,000 na wanawake
2,000. Wafungwa waliohukumiwa wako 522 kati yao wanaume ni 503 na
wanawake ni 19. Nimeamua kusamehe wafungwa 8157, ambapo baada ya msamaha
huu wafungwa 1828 watatoka leo.
“Mfano
wa watu niliowasamehe ni Mzee Mganga Matonya mwenye umri wa miaka 85
amekaa Gerezani miaka 37 na miaka 7 ya kukaa mahabusu. Nimeamua kusaheme
familia ya Nguza Viking jina lingine anaitwa Babu Seya na Ndugu Johnson
Nguza ama Papii Kocha.
“Nimeamua
kuwasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa. Lakini katika
kuchunguzwa kwingi wapo wafungwa ambao wametubu dhambi zao, wamekiri
makosa yao kwelikweli,” alisema Magufuli.
Mwaka
2003, Babu Seya na wanaye watatu walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya
kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa, mwaka 2004,
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar iliwahukumu wote wanne kifungo cha
maisha jela.
Baada
ya hukumu hiyo, walikata rufaa lakini mwaka 2005, Mahakama Kuu
iliridhia hukumu hiyo ya kifungo cha maisha jela kwa wote wanne kabla ya
Mahakama ya Rufaa kuwaachia huru Mbangu na Chichi Februari 2010.
Post a Comment
karibu kwa maoni