LIGI
ya Daraja la Nne ngazi ya wilaya msimu wa 2017/2018 inaendelea kutimua vumbi
katika viwanja vya Kata ya Gallapo wilaya ya Babati mkoani Manyara, ambapo katika msimamo wa ligi hiyo Babati Mashujaa wanaendelea kuongoza.
Wikiendi hii hapa ilishuhudiwa Town Boys wakitoshana nguvu na Vija Sc kwa bao 1-1,BM Sc wakiwaadhibu Ngurumo Sc mabao 4-0,Kariakoo wakagawa dozi ya bao 2-1 dhidi ya Town Boys,Bm Sc wakapimana nguvu na Mrara Fc 1-1.
Mwenyekiti wa chama chaa soka wilaya ya Babati Gerald Mtui amesema kuwa Ni timu sita pekee zinazoshiriki michuano hiyo ya Ligi daraja la nne ngazi ya wilaya,michuano ambayo inatambuliwa na kalenda ya shirikisho la soka Tanzania [TFF] ambazo ni Mrara Fc,Vijana Sc,Town Boys,Bm Sc,Ngurumo Sc na Kariakoo Fc.
Baada ya michezo hiyo Bm Sc inaongoza kwa alama 7 akifuatiwa na Mrara Fc wenye alama 3,Ngurumo 3,Kariakoo Fc 3,Town Boys 1 na Vijana Sc alama 1.
Timu itakayoshinda katika michezo hii ina maana kuwa itaungana na timu za Usalama Fc na Gallapo Parish kwenye ligi ya mkoa wa Manyara[ligi daraja la Tatu].

Post a Comment
karibu kwa maoni