Anaandika Beny Mwaipaja
Wizara
ya Fedha na Mipango Fungu Hamsini (Vote 50)linalohusika na masuala ya
utawala, limeibuka kinara kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza katika
utoaji wa Taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 katika kundi la
Wizara na Idara za Serikali inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi
wa
Hesabu (NBAA).
Tuzo
hizo zimetolewa kwa washindi na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis
Mwakapalila kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw.
Doto James katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo
Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa
Mkutano wa mwaka wa
Wahasibu nchini uliofanyika katika eneo hilo.
CPA.
Mwakapalila alisema kuwa taarifa bora za fedha ni muhimu sana katika maendeleo
ya nchi kwa kuwa walipa kodi, wawekezaji na wadau wengine hutegemea taarifa
hizo katika kufanya maamuzi.
‘Kama
taarifa za fedha hazitatolewa kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati mwafaka
kunaweza kusababisha athari katika uthabiti wa mifumo ya kifedha nchini’,
alieleza CPA. Mwakapalila
Aidha
Mwakapalila amewapongeza wahasibu kwa kuamua kukaa pamoja na kujadili taaluma
ya uhasibu katika maendeleo ya viwanda ambayo ni ajenda ya kipaumbele kwa
Serikali ya awamu ya tano.
Amesema
suala la Uchumi wa viwanda ni muhimu katika kuongeza kipato na kupata fedha za
kigeni kwa njia ya kuuza bidhaa nje na pia kupata mapato ya kodi na yasiyo ya
kodi hivyo akatoa rai kwa wananchi kuendelea kujadili masuala ya uchumi wa
viwanda na kupata namna sahihi ya
kuufikia ili ndoto ya uchumi huo ziweze kuwa za kweli.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA),
CPA. Pius Maneno amesema kuwa tuzo zinazotolewa na NBAA zinalengo la
kuhamasisha uwajibikaji na kuandaa taarifa ya fedha zilizo na viwango vya
kimataifa.
Amesema
kuwa washindi wa tuzo hizo wanapatikana kupitia mchakato uliosheheni weledi wa
hali ya juu kutoka kwa wabobezi wa taaluma ya uhasibu nchini ambao wanaangalia
vigezo kadhaa vikiwemo kuwa na hati safi na kuwasilisha Hesabu kwa wakati na
pia kufikisha kiwango cha ubora wa taarifa kuanzia asilimia 75.
Mhasibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50, Bw. Christopher Nkupama,
amesema kuwa tuzo hiyo inawapa morali ya kufanyakazi kwa umahili zaidi
na kuwapongeza watumishi walioko katika idara yake kwa kufanyakazi kubwa
na bila kuchoka kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni na taratibu za
uhasibu wanapotekeleza majukumu yao.
Mshindi
wa Jumla katika tuzo hizo kwa taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 ni Twiga
Cement Plc na kwa upande wa Wizara na Idara za Serikali ni Wizara ya Fedha na
Mipango fungu hamsini (V. 50), tuzo ambayo ilipokelewa na Mhasibu Mkuu wa fungu
hilo Bw. Christopher Nkupama, ikifuatiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji fungu arobaini na nne (V.44) na Ofisi ya Waziri Mkuu fungu ishirini
na tano (V. 25)
Washiriki
wa Tuzo hizo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Wakala wa Serikali, Wizara na
Idara za Serikali na Sekta Binafsi ambapo kwa mwaka huu waliojitokeza kutoka
Mamlaka ya Serikali za Mitaa walikua sita na Wizara na Idara za Serikali
walikua sita.
Jumla
ya washidani waliojitokeza ni 56 na waliofanikiwa kuvuka kigezo cha kuwa na
zaidi ya asilimia 75 walikua washidi 36 na hao walifanikiwa kushika nafasi ya
kwanza hadi ya tatu kulingana na makundi.
Vilevile
Idadi ya Wahasibu ambao wamehudhuria katika Mkutano wa mwaka ambao hufanyika
kila mwaka kabla ya kutolewa tuzo hizo imepanda kwa asilimia 60 ambapo mwaka
2016 walihudhuria wajumbe 1700 ilihali mwaka huu 2017 wamehudhuria zaidi ya
wajumbe 2700.
Post a Comment
karibu kwa maoni