Treni
ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania iliyokuwa ikitokea mkoani Dodoma
kwenda Kigoma imepata ajali katika eneo la Kijiji cha Mpeta wilayani
Uvinza.
Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na kusababisha mabehewa mawili kuanguka katika dimbwi dogo la maji.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Othieno amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo. Mpaka sasa hakuna taarifa ya vifo wala idadi ya majeruhi.
Behewa kadhaa bado zimesalia kwenye njia yake baada ya ajali.
Post a Comment
karibu kwa maoni