Wananchi
wa kijiji cha Mpanda Kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Songwe
wameshikwa na taharuki baada ya mbwa aliyewasumbua kwa siku nyingi kwa
matukio ya uhalifu hasa kwa kukamata kuku kijijini hapo kugeuka na kuwa
binadamu na kuanza kuongea.
Afisa
Mtendaji wa kijiji hicho amethibitisha tukio hilo kutokea na kuongeza
kuwa wamekumbwa natahauki kubwa kuona kitu cha ajabu binadamu
kujibadilisha kuwa mbwa na kuanza kufanya uhalifu kitu ambacho
kimewashitua wengi. Inadaiwa mbwa huyo kwa siku alikuwa anakamata kuku
kuanzia watatu mpaka wa tano.
Mmoja
wa wamashuhuda wa tukio hilo alisimulia kuwa "Kuku walianza kupotea
muda mrefu kwa hiyo tulichukua jukumu la kumtaarifa Afisa Mtendaji
kwamba kuna mbwa amemaliza kuku za wananchi kwenye kitongoji cha Mpanda
kati kwa hiyo baada ya hapo tumeamua kuamka na kuanza kufukuzana na huyo
mbwa, tulianza kufukuzana naye kuanzia saa kumi na mbili na kufika saa
nne ya asubuhi wakati tunakaribia kumkamata akabadilika na kutokea
binadamu" alieleza mwananchi
Afisa
Mtendaji aliendelea kusimulia juu ya tukio hilo na kusema baada ya mbwa
yule kubadilika na kuwa binadamu alianza kuongea akiwaomba wananchi
wamuue na kukiri kuwa yeye ni mchawi na alitumwa.
"Baada
ya hapo alijitambulisha anaitwa Happy Victor akaomba tusimrudishe kwao
Ilemi bali tumuue na kusema kuwa mtoto wake anatuachia tumle sisi
tukasema hapana hatuwezi kukuuwa ila tunakuomba utupe maelezo huku Mbozi
umekujaje akasema huku nimekuja kuna mtu amenileta ila mama yangu ni
mshirikina alichomewa nyumba kule Ilemi kwa hiyo mimi ni yule mbwa
ambaye alipotea kule Ilemi aliyekuwa anatuhumiwa kwamba anakichaa. Sisi
tukamsihi kwamba wewe basi sisi tunakuomba hizo nguo vaa akasema nikivaa
hizi nguo nitabadilika kuwa mbwa yule wa kichaa" alisema Afisa
Mtendaji
Kwa
upande wake Afisa Tarafa ya Vwawa Haji Hamisi Ibrahamu amewataka
wananchi kuachana na mambo ya kishirikina ambapo amewataka wazee wa mila
na wachungaji wakemee tukio hilo na kusema kuwa mtu huyo wao
watamfikisha kwenye vyombo vya sheria kwa kufanya uhalifu.
Post a Comment
karibu kwa maoni