Ahadi
hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jassem Ibrahim
Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango.
Balozi
Al-Najem amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na
kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati
ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya
Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.
Aliahidi
kuwa nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika (Mifuko
ya Waarabu) wa mfuko huo, wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa
ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili
iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.
Katika
kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, kupitia Kuwait Fund, imeipatia
Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni
608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara,
kilimo, umeme, Maji na Afya.
Baadhi
ya miradi hiyo ambayo imekamilika ni pamoja na barabara ya Dar es Salaam hadi
Somanga inayohusisha pia ujenzi wa Daraja la Mkapa, Kiwanda cha Karatasi
Mufindi, Mradi wa kuzalisha Umeme unaotokana na nguvu ya maji-Mtera, na gharama
za upembuzi yakinifu wa upanuzi wa Bandari ya Zanzibar.
Kwa
upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru
Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa Maendeleo wa Kuwait kwa kuisaidia nchi
kutimiza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia mikopo yenye
gharama nafuu inayotolewa na taasisi hiyo.
Dkt.
Mpango alisema kuwa mwaka jana, Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait uliipatia Tanzania
mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115
kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha
lami pamoja na mradi wa maji safi na salama wa miji ya Same na Mwanga mkoani
Kilimanjaro na sehemu ya eneo la wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wenye thamani
ya shilingi bilioni 77,
Mradi
mwingine ni ufadhili wa ukarabati wa hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar
utakaogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.