Mahakama
ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu(AfCHPR), imesema Mahakama za
ndani Tanzania katika kesi ya kubaka na kulawiti iliyokuwa inamkabili
mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na mwanawe Johnson Nguza (Papii
Kocha) zilitenda haki kwa kiwango kikubwa na kwa upande mwingine
zilikiukwa.
Aidha,
kutokana na kukiukwa kwa baadhi ya haki zao hizo, mahakama hiyo
imewaruhusu kuwasilisha hoja na kuainisha ni namna wanaweza kuomba fidia
kulingana na haki zao ziliokiukwa ndani ya siku 30 huku upande wa
Jamhuri ukitakiwa kujibu hoja hizo ndani ya siku 30.
Akitoa
hukumu hiyo katika mahakama hiyo leo Ijumaa Machi 23, Kiongozi wa
majaji nane waliokuwa wakisilikiza shauri hilo, Gerald Niyungeko mbele
ya Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Sylvain Ore, amesema baadhi ya haki
zilizotendwa ni pamoja na kuwaachia watuhumiwa watatu kwenye kesi hiyo
pamoja na kubakiza mashitaka manne kati ya 21 yaliyokuwa yakiwakabili.
“Haki
zao hazikukiukwa kulingana na uamuzi uliotolewa na mahakama za ndani za
Tanzania kwa kuwaachia washtakiwa wengine na kupunguza mashtaka 21 hadi
manne, lakini kwa upande mwingine zilikiukwa, kwa mfano wakiwa Mahakama
ya Halimu Mkazi Kisuti walikaaa mahabusu kwa siku nne bila kufahamishwa
makosa yao lakini pia hawakuwa na wakili wa kuwatetea.
“Aidha,
waleta maombi pia waliomba kupimwa mkojo na damu ili kuthibitishwa kama
waliwaingilia wale watoto ambao upande wa jamhuri ulidai waliambukizwa
magonjwa ya zinaa lakini walikataliwa.
“Kwa
upande mwingine, Nguza aliomba kupimwa kama ana uwezo wa kufanya tendo
la ndoa au lakini pia alikataliwa,” amesema Jaji Niyungeko.
Hata
hivyo, kuhusu kupinga kifungo cha maisha, Jaji Niyungeko amesema
mahakama haikujielekeza katika shauri hilo kwa sababu waleta maombi wako
huru kwa msamaha wa rais hivyo haikuona sababu ya kushughulikia hilo
kwani wako nje kwa mujibu wa sheria.
Babu
Seya na Papii Kocha waliachiwa kwa msamaha wa rais Desemba 9, mwaka
jana kutokana na kifungo cha maisha jela walichohukumiwa na Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Juni mwaka 2004 baada ya
kumkuta na hatia ya kunajisi na kulawiti watoto 10 ambapo walikata rufaa
Mahakama za juu na kugonga mwamba na hivyo kulazimika kukimbilia AfCHPR
wakidai haki zao zilivunjwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni