0

 
Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara imepitisha bajeti yake ya mwaka 2017/2018 katika kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kilichoketi leo.
Bajeti iliyopitishwa na madiwani bila kupata pingamizi lolote imetajwa kuwa  ni shilingi Bilioni sita [6].

MADIWANI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA KANUNI KATIKA VIKAO VYAO.

Hata hivyo Madiwani wamekumbushwa  kuzingatia taratibu na kanuni walizoweka katika vikao vyao ili kujadili mambo mbali mbali ya maendeleo katika kata zao kwa ufasaha.

Hayo yamesisitizwa leo na mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Kibiki Mohamedi ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Baraza la madiwani Babati mji katika Kikao cha madiwani  kilichofanyika kwa siku  mbili katika ukumbi wa wa mikutano wa  Halmashauri hiyo.

Kikao hicho cha baraza la madiwani ni cha robo ya pili ya mwaka 2017/2018.
Diwani wa kata ya Maisaka Abrahman Kololi alionekana kuzungumza kwa jazba wakati wa kupitia baadhi ya vifungu kwa kueleza kuwa mapendekezo yaliyopo katika kutekeleza miradi  mbalimbali ya mji wa Babati kata yake haikupewa kipaumbele.
Diwani kata ya Maisaka Abrahaman Kololi [CHADEMA]

Hali hiyo ya mvutano wa maneno Mheshimiwa Kololi na mwenyekiti wa baraza hilo Mohamedi Kibiki  ilipelekea kurushiana maneno kiasi cha kutaka hata kurushiana ngumi kama wangesogeleana.

Kumbuka kuwa baraza hilo linatawaliwa kwa kiasi kikubwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA]yenye madiwani wtano huku Chama Mapinduzi [CCM] ina idadi ya madiwani wanne.
Kama kawaida katika kikao hicho cha madiwani walikuwepo pia watumishi kutoka katika idara mbalimbali.
Wajumbe wakifuatilia kwa makini mada katika baraza la madiwani Mjini Babati

Wajumbe wakifuatilia kwa makini mada katika baraza la madiwani Mjini Babati


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top